Pichani juu ni mwaka 2015, wakati Deus Kaseke akitambulishwa na Afisa Habari wa Yanga Jerry Murro baada ya kusajiliwa.
Kiungo mshambuliaji wa Singida United Deus Kaseke aliitumikia Yanga kwa misimu miwili kabla hajaondoka msimu wa 2017/18 kuuungana na Hans van Pluijm katika klabu ya Singida United.
Pluijm ndiye aliyemsajili kutoka klabu ya Mbeya City.
Kaseke amekuwa katika kiwango bora katika klabu ya Singida United msimu uliomaliza.
Hakuna shaka yeye ndiye aliyen'gara zaidi kwenye michuano ya SPortPesa Super Cup kwa wachezaji kutoka timu za Tanzania.

Kwenye mchezo wa kusaka mshindi wa tatu kati ya Singida United dhidi ya KK HomeBoyz, Kaseke alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo na jopo la wakufunzi kutoka Akademi ya klabu ya Everton na kukabidhiwa tuzo hiyo na nyota wa zamani wa timu ya Taifa ya Nigeria na Everton, Yakubu Ayegben.
Sifa moja ya kubwa ya Kaseke awapo dimbani ni kujituma. Kaseke ni miongoni mwa wachezaji wachache ambao hawakupi chini ya asilimia 70 ya uwezo wao kwenye michezo yote wanayocheza.
Kwa lugha nyepesi Kaseke sio mchezaji wa mechi, kwani kuna wachezaji wanan'gara kwenye baadhi ya michezo huku wakifanya vibaya kwenye michezo mingine.

ADVERTISE HERE