Ijumaa ijayo, Juni 15 2018, ndio siku ambayo dirisha la usajili kwa ajili ya msimu wa 2018/19 litafunguliwa rasmi na huenda likafungwa Agosti 06 kama ilivyokuwa kwa misimu miwili iliyopita.
Uongozi wa Yanga kupitia kwa Katibu wake Mkuu, Charles Mkwasa umesema utaanza kuanika silaha zake hadharani baada ya kufunguliwa kwa dirisha la usajili.
Wakati timu nyingine zikitangaza wachezaji zinazowasajili licha ya dirisha la usajili kuwa bado halijafunguliwa, Yanga imekuja na utaratibu tofauti msimu huu.
Katika moja ya mahojiano yake hivi karibuni, Mkwasa alisema moja ya changamoto wanayokutana nayo msimu huu ni baadhi ya timu kufanya usajili kwa kufuata 'kivuli' cha Yanga.
"Baadhi ya timu zimekuwa zikisikiliza sisi tunataka kumsajili nani kisha wanawarubuni wachezaji tunaokuwa katika mazungumzo nao na kuwasajili."
Kauli hiyo ya Mkwasa imedhirika kwa baadhi ya usajili uliofanywa na klabu ya Simba kwa Adam Salamba na Mohammed Rashid ambao Yanga ilikuwa ya kwanza kuzungumza nao.
Pia Tiber John aliyesajiliwa na Singida United.
Baada ya Mkutano Mkuu wa Wanachama uliofanyika juzi, Yanga iliunda Kamati Maalum ya kusimamia masuala ya usajili na mikataba ya wachezaji.
Sasa masuala yote ya usajili yatasimamiwa na Kamati hiyo inayoongozwa na Abbasi Tarimba akisaidiwa na Said Mecky Sadiq.
Kamati hiyo imeondoa hofu iliyokuwa imewajaa WanaYanga kwani sasa wana uhakika Yanga haitashindwa kumsajili mchezaji wanayemtaka.
Inaelezwa tayari Kamati hiyo ina fungu la kutosha kukamilisha masuala ya usajili.
Jana Mwenyekiti wake Abbas Tarimba alisema kazi ya kwanza kuifanya ni kuhakikisha wanawasainisha mikataba wachezaji wote watakaobaki Yanga kwa ajili ya msimu ujao.
Tarimba alisema kwa mujibu wa taarifa waliyopewa, ni wachezaji saba tu waliokuwa na mikataba katika klabu ya Yanga.
Baada ya zoezi hilo Tarimba alisema litafuata zoezi la usajili wa wachezaji wapya. Zoezi ambalo litazingatia mahitaji ya klabu ya Yanga.
Tarimba amesisitiza wamedhamiria kuirudisha heshima ya Yanga iliyotetereka msimu uliomalizika.

ADVERTISE HERE