Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua alipata majeraha kwenye mchezo uliopita dhidi ya Azam Fc akitarajiwa kufanyiwa vipimo zaidi kubaini ukubwa wa majeraha hayo.
Kamwe amesema Pacome aliumizwa kwenye mchezo huo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 huku akishangaa tukio la faulo alilofanyiwa na Lusajo Mwaikenda mapema kwenye kipindi cha kwanza kuchukuliwa la kawaida.
"Pacome aliumia sana kwenye mchezo dhidi ya Azam Fc, nashangaa sijasikia mijadala yoyote kutoka kwa wachambuzi. Alifanyiwa rafu mbaya lakini alijikaza tu kumaliza mchezo"
"Baada ya mchezo tulimuona akichechemea, alitarajiwa kufanyiwa vipimo zaidi kubaini ukubwa wa jeraha hilo," alisema Kamwe.
Adha Kamwe amethibitisha kuwa mlinzi wa kulia Yao Kouassi 'Jeshi' nae alipata majeraha madogo ambayo tayari ametibiwa na anaweza kuwa tayari kuikabili TRA United siku ya kesho.
Pacome alifunga bao la tatu kwenye mchezo huo uliopigwa uwanja wa New Amaan Complex, visiwani Zanzibar.
Msimu huu Pacome ameandamwa na majeraha ya mara kwa mara ambayo yamemfanya akose baadhi ya mechi muhimu.
Wakati mwingine Profesa huyo wa mpira alilazimika kucheza akiwa na maumivu ili tu kuhakikisha anaisaidia timu yake kupta alama tatu