Kesho Jumamosi, Juni 27 2026 Yanga inarejea uwanja wa nyumbani, KMC Complex pale itakapoikaribisha TRA United katika mchezo wa ligi kuu ya NBC, Mzunguuko wa 29.
Ni moja kati ya mechi mbili zilizobaki kuhitimisha msimu Yanga ikihitaji ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi dimba la KMC Complex kuipa hamasa timu yao katika mchezo ambao Wananchi wanahitaji matokeo ya aina moja tu, USHINDI.
Yanga imetangaza viingilio vya mchezo huo utakaopigwa saa 10 jioni.

ADVERTISE HERE