Licha ya kutofunga bao, mshambuliaji Prince Dube ameibuka nyota wa mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga dhidi ya Azam Fc uliopigwa uwanja wa New Amaan Complex na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.
Dube alionyesha kiwango bora katika mchezo huo akihusika kwenye mabao mawili kati ya matatu yaliyofungwa.
Krosi yake dakika ya 41 ilijazwa kambani na beki Ibrahim Bacca huku shuti lake dakika ya 81 awali likigonga mwamba na kurejea tena kwake akapiga mara ya pili mlinda lango Zuberi Foba akiokoa na kumtengea Pacome Zouzoua aliyefunga bao la tatu.
Mkufunzi wa Yanga Abdihamid Moalin leo aliwaanzisha wote Depu na Dube uamuzi ambao kwa kiasi kikubwa uliinufaisha Yanga Dube akiwapa wakati mgumu walinzi wa Azam Fc.
Katika nyakati ambazo anapambana kurejesha makali yake kwenye kuzifumania nyavu, asisti zake zimekuwa na thamani kubwa kwa ushindi wa Yanga leo.
