Yanga leo imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Azam Fc katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar.
Ushindi huo umeendelea kuweka salama malengo ya Yanga kutetea ubingwa kwa msimu wa tano mfululizo sasa wakihitaji kukamilisha kazi hiyo kwenye mechi mbili zilizobaki.
Haikuwa rahisi kwa Yanga kupata ushindi huo, kulikuwa na mapambano makali ndani ya uwanja na kama sio kujitoa kwa wachezaji pengine mambo yangekuwa magumu.
Sifa za kipekee zinakwenda kwa mlinda lango Djigui Diarra 'Mdaka Mishale' leo amehakikisha anaondoka na cleansheet.
Diarra alifanya kazi kubwa akiokoa michomo kadhaa iliyoelekezwa langoni na kuiweka Yanga salama kwa muda wote wa mchezo.
Leo Diarra amejihakikishia tuzo ya golikipa bora wa msimu baada ya kufikisha cleensheet ya 16.
Zikiwa zimesalia mechi mbili, hakuna mlinda lango mwingine ambaye anaweza kufikisha cleensheet 16.