Kiungo mshambuliaji wa Yanga Celestin Ecua amekamilisha muda wake wa mkopo kunako klabu ya JS Kabylie.
Klabu hiyo kutoka Algeria imethibitisha kuachana nae baada ya muda huo wa mkopo kumalizika.
Kabylie walikuwa na makubaliano na Yanga ya kumnunua moja kwa moja Ecua kama wangeridhishwa na uwezo wake.
Ni rasmi sasa Ecua anarejea Yanga ambako hata hivyo inaelezwa uongozi huenda ukasitisha mkataba wake kwa makubaliano ya pande mbili kwa sababu hayupo kwenye mipango ya mabingwa hao wa soka Tanzania Bara kuelekea msimu ujao.
Ecua alitua Yanga kwenye dirisha kubwa lililopita akitokea klabu ya Asec Mimosas, hata hivyo alishindwa kuonyesha makali yake na kupelekea akatoleewa kwa mkopo mwezi Januari

ADVERTISE HERE