Kiungo kiraka wa Yanga Duke Abuya jana aliondoka na tuzo ya nyota wa mchezo baada ya 'kukiwasha' kwelikweli kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Fountain Gate uliopigwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Katika mchezo huo ambao Yanga waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi, Abuya aling'ara eneo la kiungo akianza kama kiungo mkabaji na baade kusogea namba 8 alipoingia Mohamed Damaro.
Ni kama Abuya 'ana-enjoy' mechi dhidi ya Fountain Gate kwani katika mechi ya duru ya kwanza iliyopigwa mwaka jana Abuya aliondoka na tuzo ya nyota wa mchezo huku Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Hivyo alichofanya jana ni kama amerudia kile alichofanya mwaka uliopita dhidi ya timu ileile..1


ADVERTISE HERE