Wakati Wananchi wakifurahia ushindi wao wa 20 msimu huu, kuna kazi kubwa inafanywa na wachezaji kuhakikisha wanaendelea kufurahi.
Mlinda lango Djigui Diarra ameendelea kuwa nguzo muhimu ya mafanikio ya Yanga akiendelea kuliweka salama lango kwa kushirikiana na wenzake wa safu ya ulinzi.
Diarra leo amehakikisha nyavu zake ziko salama kwa muda wote wa mchezo wakati Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Fountain Gate.
Ziko nyakati Diarra alilazimika kufanya kazi ya ziada akiokoa michomo mikali langoni.
Diarra anaendelea kuongoza orodha ya vinara wa cleensheet akifikisha 15.
Msimu huu Diarra anataka kurejesha tuzo ya mlinda lango bora aliyoipoteza msimu uliopita.
ADVERTISE HERE