Barua ya wazi kwa Mzee Akilimali

Yanga Damu By Yanga Damu
β€’
11 Jun 2018
Barua ya wazi kwa Mzee Akilimali
Mwaka jana, Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji aliandika barua ya kuomba ajiuzulu nafasi yake.

Katiba ya Yanga inaelekeza utaratibu wa kufuatwa kuwa ni lazima barua hiyo iwasilishwe mbele ya wanachama kupitia Mkutano Mkuu kwa ajili ya kujadiliwa kisha kutolewa maamuzi.

Barua hiyo haikuwahi kujadiliwa, hivyo jana Wanachama walipata nafasi ya kuijadili kama Katiba inayoelekeza

Kwa kauli moja, Wanachama wa Yanga kupitia Mkutano huo, hawajaridhishwa na sababu zilizotolewa na Manji juu ya kujiuzulu kwake hivyo wamekataa maombi yake na kumtaka aendelee na wadhifa wake.

Hapa mimi silioni kosa la Wanachama zaidi ya kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa Katiba.

Mzee Akilimali kumbuka Manji ni Mwenyekiti halali wa Yanga kwani alichaguliwa na wanachama kupitia Mkutano halali, Muda wake unamalizika mwaka 2020.

Kama wanachama wengi wameridhishwa na uongozi wake na wamependa aendelee basi we ni nani kupinga maamuzi hayo?

Swala la kuwa amekaa nje mwaka mzima sio hoja, kwa kuwa maombi yake ilikuwa ni lazima yakajadiliwe kwenye mkutano mkuu ambao haukuwa umefanyika.

Malalamiko yako yangekuwa ya msingi kama Manji angekuwa amekataa maombi yao na bado wanachama wakaendelea kulazimisha arejee.

Manji bado hajatoa kauli yake juu ya maazimio ya kumtaka arejee yaliyofikiwa na wanachama kwenye Mkutano Mkuu hapo jana, wewe tatizo lako ni nini?

Kwani Mzee Akilimali huyu bwana Manji amekukosea nini mpaka uwe unampinga tu bila sababu za msingi?

Mwanzo ulipinga mpango wake wa kuikodisha Yanga. Na ukasisitiza kwamba Yanga haiwezi kukodishwa kama 'masufulia ya shughuli'.

Wapo wengi waliokuunga mkono kwa sababu walidhani ulikuwa na sababu za msingi sana.

Lakini kumpinga kwako Manji wakati huu kunashangaza sana kwa kuwa hata kama akirejea sasa harudi na mpango wa kukodisha timu, bali anarudi katika nafasi yake halali ya Uwenyekiti ambayo alichaguliwa na Wanachama.

Na hata kama akitaka kuwekeza katika klabu ya Yanga, atafuata utaratibu mpya wa uwekezaji uliopendekezwa na Serikali ambao tayari ulishapitishwa na wanachama kwenye Katiba ya Yanga.

Wewe Mzee Akilimali umekiri kuunga mkono utaratibu huu mpya wa uwekezaji kwa maslahi mapana ya klabu ya Yanga.

Sasa iweje leo unapinga kurejea kwa Manji ambaye hakuna shaka amekuwa kinara wa mafanikio ya klabu ya Yanga kwa zaidi ya miaka 10?

Au unapenda Yanga iendelee kutaabika na hali iliyoikumba msimu huu?

Mzee Akilimali ngoja nikwambie, mpira wa karne hii unahitaji uwekezaji mkubwa. Ili tufanikiwe lazima timu tuziweke mikononi mwa watu wenye weledi na uwezo wa kifedha.

Mzee Akilimali tukikukabidhi timu wewe leo nakwambia hutaweza, utatukimbia kama wakati huu ulivyotuacha tunataabika.

Sisi wanachama tumekuwa na timu kwa zaidi ya miaka 80 lakini tumefanya nini?

Tuungane pamoja kuijenga Yanga imara, tuache makundi na kupinga kila jambo kwa sababu binafsi zisizo na mashiko.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
12h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
16h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
17h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
17h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’