Kikosi cha Yanga kimeondoka jijini Dar es salaam kuelekea mkoani Arusha tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Fountain Gate.
Siku ya Alhamisi, Juni 18 2026 Yanga itashuka dimba la Sheikh Amri Abeid kuwakabili wenyeji wao Fountain Gate katika mchezo utakaopigwa saa 10 jioni.
Kuanzia Alhmisi, Yanga inakabiliwa na mfululizo wa mechi zitakazopigwa kila baada ya siku tatu hadi mwisho wa msimu.
Baada ya mchezo dhidi ya Fountain Gate, Yanga itaelekea jijini Mwanza kuikabili Azam Fc kwenye mchezo wa nusu fainali kombe la CRDB utakaopigwa Juni 21 katika uwanja wa CCM Kirumba.
Yanga na Azam Fc zitachuana tena Juni 24 kwenye mchezo wa ligi kuu utakaopigwa uwanja wa New Amaan COmplex visiwani Zanzibar.
Juni 27 Yanga itakuwa uwanja wa KMC Complex kuikabili TRA United na Wananchi watahitimisha msimu wa ligi kuu Juni 30 kwa mchezo dhidi ya JKT Tanzania.