Kiungo mshambuliaji wa Yanga Mudathir Yahya leo ameondoka na tuzo ya nyota wa mchezo baada ya kuwaongoza Wananchi kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mashujaa Fc katika mchezo uliopigwa uwanja wa Lake Tanganyika.
Mudathir alifunga bao la kwanza la Yanga kwa shuti la nje ya 18, moja ya mabao bora yaliyofungwa kwenye ligi msimu huu.
Hilo lilikuwa bao lake la 9 kwenye ligi Muda sasa akimfikia mshambuliaji Prince Dube ambaye amesimama kwenye mabao 9 kwa muda mrefu/
Ni msimu mwingine wa mafanikio kwa Mudathir akiendeleza takwimu bora kwenye kufunga licha ya eneo analocheza.

Β
ADVERTISE HERE