Gor Mahia imefanikiwa kutwaa taji la SportPesa Super Cup kwa msimu wa pili mfululizo baada ya kuilaza Simba mabao 2-0 kwenye mchezo wa fainali uliopigwa kwenye uwanja wa Afraha, Nakuru.
Washambuliaji Meddy Kagere na Jack Tuyisenge ndio walioifungia Gor mabao yote katika mchezo ambao watani zetu wametia aibu kwani walizidiwa kila idara.
Yanga itachuana na Gor Mahia Julai 18, 2018 kwenye mchezo wa tatu wa kombe la Shirikisho nchini Kenya kisha kurudiana nao siku 10 baadae jijini Dar es salaam.
Kwenye michuano hii ya SportPesa Gor Mahia imeonyesha kiwango cha hali ya juu, hakika yapasa kujipanga kwelikweli kuweza kuwafunga.
Mshambuliaji wao Meddy Kagere ameibuka kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo baada ya kufunga mabao manne kutoka michezo mitatu aliyocheza.
Benchi la ufundi la Yanga litakuwa na kazi ya ziada kuhakikisha linaandaa kikosi imara kitakachoweza kupambana na wababe hao wa soka la Kenya ambao hawajapoteza mchezo kwenye dimba lao mwaka 2018.

ADVERTISE HERE