Tambo za Julio kuelekea mchezo dhidi ya Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
10 Jun 2026
Tambo za Julio kuelekea mchezo dhidi ya Yanga

Kocha wa Mashujaa FC, Jamhuri Kiwhelo maarufu kama “Julio”, ametoa kauli zenye kuonyesha kujiamini kupita kiasi kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Yanga SC, utakaopigwa Jumamosi katika Uwanja wa Lake Tanganyika.

Julio amesema kuwa mabingwa watetezi wa ligi hiyo hawatakumbana na mchezo mwepesi, akisisitiza kuwa kikosi chake kimejiandaa vya kutosha kuhakikisha hakiruhusu ushindi wa kirahisi kama ilivyotokea katika michezo ya nyuma.

Akizungumza kwa msisitizo, kocha huyo amesema anaifahamu vyema Yanga, lakini pia anaamini hata wapinzani wake hao wanatambua ugumu wa mchezo watakaokutana nao.

Julio amesema katika historia yake ya ukocha na makocha aliofanya nao kazi, amekuwa na rekodi ya kuweza kupata matokeo dhidi ya timu kubwa, akisisitiza kuwa imani yake haijabadilika hata anapokutana na mabingwa hao watetezi.

"‎Mimi nafikiri kila mtu ana philosophy yake. Philosophy yangu mimi kufungwa tano na Yanga itakuwa sio kazi rahisi kwasababu Yanga sio mara yangu ya kwanza kucheza nao. Nikiwa Simba nishacheza nao na nimewafunga na kama wao wamenifunga, Sikumbuki ni lini."

"Nikiwa na Kajumulo nishawafunga, nikiwa na Mwadui nishawafunga kwahiyo bado nina rekodi ya kuwafunga Yanga. ‎ ‎Kwahiyo na wenyewe Yanga wanajua kabisa kwamba tunaenda kucheza na kocha ambaye ana confidence kuliko kitu chochote kwahiyo confidence yangu ambayo nilikuwa nayo kwa Simba ndiyo hiyo hiyo ambayo niko nayo kwa Yanga tena mimi nataka nikwambie, Simba wanaweza kuwa na forward kali kuliko Yanga."

"Yanga kwangu mimi ni timu nyepesi. ‎ ‎Nawaheshimu, wana wachezaji wazuri, Dube ni Opportunist sio Fighter, Pacome ni Dribbler mzuri anaweza akaassist na akafunga lakini wana Mudathir, mchezaji mjanja mjanja bado wana mtu kama Okello."

"Hao ukiwawekea mtu wa kuwakaba sawa sawa hawachezi, Yanga ina watu watatu tu siwezi kuwataja leo kwasababu naweza kuuza silaha lakini nakuhakikishia Yanga hawaji kufanya kazi ya kutufunga, Sio kazi rahisi. Yale mambo ya goli 5, ni zamani, sio kwa Julio." alitamba Julio

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE →
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE →
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE →
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE →
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE →
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →