Mshambuliaji wa Yanga Laurindo Aurelio 'Depu' usiku wa jana alikuwa sehemu ya kikosi cha timu ya Taifa ya Angola klichocheza mechi ya kujipima nguvu dhidi ya Afrika ya Kati.
Depu aliendeleza rekodi yake ya kuzifumania nyavu kwenye timu ya Taifa akifunga moja ya mabao katika ushindi wa mabao 3-0 kwa Angola. Pia altoa pasi ya bao la pli lililofungwa na Mabululu.
Hiyo ilikuwa mechi ya mwisho kwa Angola kuhitimisha kalenda ya FIFA na sasa Depu anarejea nchini kuendeleza mapambano ya Yanga kutetea mataji yake.
Depu anatarajiwa kurejea leo na moja kwa moja kuungana na kikosi cha Wananchi kinachotarajiwa kusafiri kuelekea mkoani Kigoma siku ya kesho Alhamisi tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mashujaa Fc utakaopigwa Jumamosi uwanja wa Lake Tanganyika.