Mlinda lango wa Yanga Djigui Diarra na kiungo mshambuliaji Allan Okello wamerejea kikosini baada ya kukamilisha majukumu ya timu za Taifa.
Wachezaaji hao wanaungana na wenzao ambao wanaendelea na maandalizi ya mechi za mwishoni mwa msimu.
Mshambuliaji Prince Dube alirejea mapema huku nahodha Bakari Mwamnyeto akirejea sambamba na wachezaji wengine waliokuwa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania.
Aidha Ibrahim Bacca, Mudathir Yahya, Ninju, Shekhan Khamis na Casemiro wao wamejumuishwa kikosi cha Zanzibar Heroes ambacho kitacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Uganda siku ya Alhamisi.
Hata hivyo chanzo kutoka ndani ya uongozi wa Yanga kimebainisha kuwa Yanga haitawaruhusu wachezaji wake kujiunga na timu ya Zanzibar Heroes kutokana na changamoto ya ratiba
Ijumaa Yanga inapaswa kuwa Kigoma tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mashujaa Fc utakaopigwa Jumamosi




