Mlinzi wa kushoto wa Yanga Chadrack Boka ni miongoni mwa wachezaji wanaomaliza mikataba mwishoni mwa mwezi huu.
Mpaka sasa bado uongozi wa mabingwa hao wa nchi haujafungua mazungumzo nae kwa ajili ya kuhuisha mkataba wake.
Wakati huohuo taarifa kutoka duru za usajili zimedokeza kuwa Yanga imefungua mazungumzo na Singida BS kupata huduma ya mlinzi wa kushoto Ibrahim Imoro.
Boka amekuwa na 'ingia-toka' nyingi kwenye kikosi cha kwanza kutokana na changamoto za majeraha ya mara kwa mara.
Pengine hiyo ndio sababu inayopelekea mabosi wa Yanga kufikiria mbadala wake ili kuhakikisha wanakuwa imara katika eneo hilo.
Katika dirisha kubwa lililopita Yanga ilimsajili Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' akitokea klabu ya Simba hata hivyo nae amekuwa nje kwa takribni wiki nne akiuguza majeraha.
Zimbwe Jr amepona majeraha na pengine ataanza kuonekana uwanjani kwenye mchezo ujao dhidi ya Mashujaa Fc wiki ijayo.