Mabosi Yanga wamtega Aziz Ki

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Jun 2026
Mabosi Yanga wamtega Aziz Ki

Kiungo mshambuliaji wa Al Ittihad, Stephane Aziz Ki, huenda akarejea tena ndani ya kikosi cha Yanga, lakini safari hiyo inaonekana kuwa na vikwazo kadhaa baada ya mabosi wa klabu hiyo kuweka wazi msimamo wao kuhusu nyota huyo.

Taarifa zinaeleza kuwa Aziz Ki ameonyesha nia ya kutaka kurejea Jangwani baada ya kupitia kipindi kigumu katika timu yake ya sasa ya Al Ittihad ya Libya. Hata hivyo, viongozi wa Yanga wameweka bayana kuwa hawapo tayari kuingia kwenye gharama za kuvunja mkataba wake uliosalia na klabu hiyo.

Badala yake, mabingwa hao wa Tanzania wamemtaka kwanza amalizane na waajiri wake wa sasa kabla ya kuanza mazungumzo rasmi ya kurejea kwenye kikosi hicho.

Hakuna shaka kuwa Aziz Ki ni mmoja wa wachezaji walioacha historia kubwa ndani ya Yanga katika miaka ya hivi karibuni. Ndani ya misimu mitatu aliyocheza Jangwani, alifanikiwa kuwa miongoni mwa nyota waliobadilisha sura ya timu hiyo ndani na nje ya Tanzania.

Msimu wa 2022/23 aliibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara akiwa na mabao 21, huku pia akichangia kwa kiwango kikubwa Yanga kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika. Rekodi zake na uwezo wake wa kutengeneza na kufunga mabao vilimfanya kuwa mmoja wa viungo bora katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Kutokana na mchango huo mkubwa, viongozi wa Yanga wanaonekana kutofunga mlango kwa nyota huyo. Badala yake, wameweka mazingira yanayoweza kumruhusu kurejea iwapo atakuwa huru kimkataba.

Chanzo kikubwa cha kutaka kuondoka Libya kinatajwa kuwa sababu za kiusalama pamoja na masuala ya kifamilia. Tangu afunge ndoa na mwanamitindo maarufu wa Tanzania, Hamisa Mobetto, imeelezwa kuwa mazingira ya sasa hayajampa utulivu wa kutosha.

Aidha, baada ya kuondoka Yanga kwa kishindo na kujiunga na Wydad Casablanca ya Morocco mwaka 2025, mambo hayakwenda kama wengi walivyotarajia. Ndani ya miezi michache nchini Morocco, Aziz Ki alishindwa kurudia makali aliyoyaonyesha Tanzania kabla ya kuhamia Al Ittihad ya Libya.

Takwimu zinaonyesha kuwa baada ya kufunga mabao 39 akiwa Yanga katika misimu mitatu, alifanikiwa kufunga bao moja pekee akiwa Wydad kabla ya kuhamia Libya.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
7h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
15h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
22h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’