Kiungo mshambuliaji wa Yanga Allan Okello alikuwa 'on-fire' mwezi May akiweka rekodi ya aina yake kwenye kikosi cha Yanga katika mechi alizocheza.
Pamoja na ushindani mkali kutoka kwa kiungo wa Azam Fc Feisal Salum na kiungo wa Simba Clatous Chama, takwimu za Okello zinambeba na pengine kustahili kushinda tuzo hiyo ambayo mpaka sasa bado haijatangazwa na Bodi ya ligi.
Okello alicheza mechi 6, akafunga mabao 9 na kutoa pasi moja ya bao. ndiye mchezaji aliyefunga mabao mengi May huku akiweka rekodi ya kufunga mabao mawili katika mechi nne mfululizo.
Fei Toto yeye alifunga mabao 7 na kutoa pasi 1 ya bao wakati Chama akifunga mabao 5 na kutoa asisti 4. Okello amehusika katika jumla ya mabao 10, Chama mabao 9 na Fei Toto mabao 8.
Upande wa nidhamu, Okello hakupewa kadi yoyote mwezi May wakati Fei Toto na Chama kila mmoja ana kadi ya njano. Hivyo kwa kigezo cha takwimu, ni wazi Okello anastahili kushinda tuzo hiyo

Ikumbukwe pia Okello alitua Yanga mwezi Januari lakini tayari takwimu zake zinampa sifa ya kuwania hata tuzo ya mchezaji bora wa msimu.
Amefunga jumla ya mabao 11 akitoa pasi 7 za mabao akiwa nyuma ya Fei Toto aliyepachika mabao 14 na kutoa pasi 8 za mabao.