Asubuhi ya leo Yanga ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Moro Kids , mchezo ukipigwa Uwanja wa Seminari, Bigwa, Morogoro.
Yanga imewalaza vijana hao chipukizi mabao 5-0.
Donald Ngoma alifunga mabao mawili, Amissi Tambwe moja na viungo Raphael Daudi na Yussuf Mhilu nao kila mmoja akafunga bao moja.
Wachezaji wote waliopo kambini na Yanga katika hoteli ya B-Z eneo la Nane Nane mjini Morogoro walipewa nafasi ya kucheza mechi hiyo, kasoro kiungo mshambuliaji Mzambia Obrey Chirwa na winga mzawa, Geoffrey Mwashiuya ambao ni majeruhi.

ADVERTISE HERE