Jamani tuleteeni Himid Mao

Admin By Admin
β€’
17 Jun 2017
Jamani tuleteeni Himid Mao
Nimesikia uongozi unatafuta namna ya kupata sahihi ya kiungo mkabaji wa Azam FC Himid Mao Mkami 'Ninja', hilo ni jambo jema sana.

Naambiwa Mao anamaliza mkataba wa kuitumikia Azam FC mwezi Novemba lakini sasa hana hamasa yakuendelea kubaki Azam kwa hata mwezi mmoja zaidi.

Kitendo cha Azam FC kushindwa kuwabakisha wachezaji wakongwe na kuwaachia waende kujiunga na Simba kimewakera wengi akiwemo yeye.

Mao anataka kuvunja mkataba wake na Azam ili aangalie mustakabali wake, akifanya hivyo anaweza kupatikana.

Kwa muda mrefu Yanga ina tatizo la kiungo mkabaji. Tangu kuondoka kwa fundi Athumani Iddi Chuji hatujabahatika kumpata mchezaji mwenye uwezo kama wake.

Frank Domayo alijaribu lakini nae baada ya kuondoka imekuwa majanga.

Said Juma 'Makapu' na Justice Zulu wameshindwa kuitendea haki nafasi hiyo.

Yanga inamuhitaji mchezaji kama Himid Mao katika nafasi hiyo. Kama Mao akipatikana, atatoa nafasi kwa viungo mafundi Thaban Kamusoko na Haruna Niyonzima kujikita zaidi katika kutengeneza nafasi za magoli kuliko kurudi sana chini kusaidia ulinzi.

Zulu ni mzuri kwenye kuucheza mpira lakini sio mzuri kwenye ukabaji na ndio maana wakati mwingine Lwandamina alikuwa akimtumia katika nafasi ya Niyonzima/Kamusoko walipokosekana.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
23h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’