Kiungo mshambuliaji wa Yanga Allan Okello amechaguliwa na Fortbet Real Stars ya Uganda kuwa mchezaji bora wa mwezi wa tano baada ya kiwango bora sana alichokionesha akiwa na mabingwa wa Tanzania, Yanga.
Fortbet Real Stars Sports ni taasisi maalum ya kimichezo nchini Uganda inayojihusisha na utoaji wa tuzo kwa wanamichezo mbalimbali wa Uganda waliofanya vizuri ndani ya mwezi husika.
Tuzo hizo zinahusu nyanja zote za michezo kuanzia wacheza mpira, wanariadha na michezo mingine.
Tuzo ya Okello imechukuliwa na mwakilishi wake, Sultan Atuko yeye akiwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya Uganda akijiandaa na mechi za kirafiki nchini Morocco. Miongoni mwa mechi hizo watacheza dhidi ya Tanzania.

ADVERTISE HERE