Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali amesema anaunga mkono mabadiliko yanayokwenda kufanywa na klabu hiyo leo.
Kwa miaka mingi, Mzee Akilimali amekuwa akipinga mabadiliko ambapo mwaka jana ndiye aliyekuwa kinara wa kumpinga aliyekuwa Mwenyekiti na Mfadhili wa Yanga, Yusuph Manji alipokuja na mpango wa kukodisha nembo ya Yanga.
"Mimi naunga mkono kwa asilimia 100 mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu ya Yanga kama ulivyopendekezwa kwenye Katiba yetu," amesema Mzee Akilimali.
"Kwa sasa hatuwezi kufanikiwa kama tutaendelea na mfumo tulionao. Yaliyotukumba msimu huu yametufunza jambo. Hayapaswi kutokea tena."
Wanachama wa klabu ya Yanga leo wanatarajia kupitisha Maazimio ya kubadili mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo kuwa Kampuni.
Wawekezaji wataruhusiwa kumiliki hadi asilimia 49 za hisa katika kampuni ya Yanga wakati Wanachama watabaki na hisa asilimia 51.

ADVERTISE HERE