Ukizungumzia wachezaji wa kigeni ambao ni kama wamekunywa 'maji ya bendera' ya Yanga, basi hutakosa kumtaja Yao Kouassi 'Jeshi'.
Yao ni mchezaji ambaye anapokuwa uwanjani basi atamwaga jasho jingi kwa ajili ya Yanga. Na hata anapokuwa nje utaona jitihada zake katika kuwahamasisha wachezaji wenzake.
Yeye na Djigui Diara ni wachezaji mfano wa wapambanaji ambao wako tayari kuifia jezi ya Yanga.
Akiwa amerejea kikamilifu kwenye fitness yake baada ya majraha yaliyomuweka nje kwa zaidi ya miezi sita, Yao amerejesha ile heshima aliyoiweka wakati alipotua kwa Wananchi misimu miwili iliyopita na kupachikwa jina la Jeshi.
Huyu ni wa kulinda kwa wivu mkubwa sana..!



ADVERTISE HERE