Ni dakika 450 za jasho na damu kwa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 May 2026
Ni dakika 450 za jasho na damu kwa Yanga

Nyota wa Yanga ambao hawana majukumu ya timu za Taifa wanaendelea na mapumziko baada ya mfululizo wa mechi.

Jumatatu Juni 1 kikosi kinatarajiwa kurejea mazoezini kwa ajili ya maandalizi ya mechi za kuhitimisha msimu.

Yanga ina mechi tano ngumu za kuhakikisha wanatetea taji la ligi kuu kwa msimu wa tano mfululizo.

Kwa jinsi msimamo ulivyo, Yanga haipaswi kupoteza zaidi ya alama 13 ili kuwa na uhakika wa ubingwa pasipo kujali matokeo ya wapinzani. Ni wazi zitakuwa dakika 450 za jasho na damu kuhakikisha taji linarejea Jangwani.

Wengi wanazitaja mechi dhidi ya Azam Fc, TRA United na JKT Tanzania kuwa ndio ngumu zaidi lakini ukweli ni kwamba hata Mashujaa Fc na Fountain Gate zitakuwa mechi ngumu.

Ni mechi mbili za ugenini ambazo Yanga itahitaji alama zote 6 kabla ya kurejea Dar kukamilisha mechi nyingine tatu.

Aidha ikumbukwe Yanga itacheza na Azam Fc mara mbili mechi ambazo zitafuatana. Watacheza Juni 21 nusu fainali ya kombe la CRDB na Juni 24 mechi ya ligi kuu ya NBC.

Baada ya mchezo huo watacheza dhidi ya TRA United na kisha kumalizana na JKT Tanzania. Hakuna nafasi ya makosa kwani kama Yanga itadondosha zaidi ya alama 2 kwenye mechi hizo huenda ikafungua mlango kwa wapinzani kutwaa ubingwa endapo watashinda mechi zao zote.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
2h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
6h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
21h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’