Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Edmund John, ni miongoni wa wachezaji wenye vipaji vikubwa akitabiriwa kufanya makubwa kwenye soka la Tanzania na hata Kimataifa siku za usoni.
Edmund alitua Yanga mwanzoni mwa msimu huu akitokea klabu ya Singida BS. Hajaonekana sana uwanjani pengine kutokana na changamoto ya jeraha la bega ambalo lilimuweka nje kwa muda mrefu.
Meneja wa Digitali wa Yanga Privaldinho amesema Edmund amedhihirisha kuwa mchezaji mwenye kipaji kikubwa akiendelea kukua na kupata uzoefu zaidi ndani ya kikosi cha Yanga.
“Kwa wachezaji wetu wengi tulio nao wenye vipaji kama taifa, basi Edmund ni miongoni mwa vijana hao. Ana kipaji kikubwa na tayari amepata exposure ya kutosha"
“Umri wake unamruhusu kufanya makubwa. Bado ana muda wa kutosha wa kuendelea kuimarika, na naamini platform ya Yanga ni sehemu sahihi kwake kuonyesha uwezo wake,” alisema Privadinho.
Tangu ujio wa kocha Abdihamid Moalin, Edmund amekuwa akipata nafasi kwenye kikosi cha kwanza mara kwa mara hatua ambayo itazidi kumuimarisha na kumpa uzoefu zaidi
Yanga imeendelea kuwa sehemu muhimu kwa maendeleo ya vijana wengi wenye vipaji nchini.