Uongozi wa klabu ya Yanga ulitoa mapumziko ya siku 6 kwa wachezaji baada ya mchezo dhidi ya Namungo Fc ambao Wananchi waliibuka na ushindi wa mabao 3-1.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa mabingwa hao wa nchi Ali Kamwe amesema kikosi kitarejea mazoezini Jumatatu Juni 1 kwa ajili ya maandalizi ya mechi za kuhitimisha msimu.
Mechi tano za ligi kuu zimesalia pamoja na mchezo wa nusu fainali kombe la CRDB dhidi ya Azam Fc.
Baada ya mapumziko ya kalenda ya FIFA, Yanga itasafiri mkoani Kigoma kuikabili Mashujaa Fc Juni 13 kisha kuelekea mkoani Arusha kuikabili Fountain Gate Juni 17.
Juni 21 Wananchi watakuwa mkoani Mwanza kuikabili Azam Fc nusu fainali ya kombe la CRDB kisha huenda wakashuka tena uwanja wa CCM Kirumba kuikabili Azam Fc kwenye mchezo wa ligi kuu Juni 24.
Juni 27 Yanga itamalizana na TRA United dimba la KMC Complex na kuhitimisha msimu dhidi ya JKT Tanzania uwanja wa Isamuhyo Juni 30