Taarifa kutoka vyanzo vya uhakika ndani ya uongozi wa Yanga ni kuwa mchakato wa kumrejesha kiungo mshambuliaji Stephan Aziz Ki umefikia hatua nzuri.
Aziz Ki ambaye kwa sasa anaitumikia Al Ittihad ya Libya, ameutaarifu uongozi wa Yanga juu ya kusudio lake la kurejea nchini ili aungane na familia yake.
Lakini pia hofu ya usalama nchini Libya imemfanya nyota huyo wa Kimataifa wa Burkina Faso kutaka kuondoka nchini humo licha ya kujiunga na Al Ittihad mwaka huu kwenye usajili wa dirisha dogo.

Hii ni bahari njema kwa Wananchi kwani urejeo wa Aziz Ki unakwenda kuimarisha zaidi eneo la kiungo cha ushambuliaji ambalo kwa sasa Wananchi wanafurahia kazi inayofanywa na Allan Okello.
Inaweza kuwa habari mbaya kwa timu pinzani kwani wakati huu wanateseka na Okello, wanafahamu vyema uwezo wa Aziz Ki na kile anachoweza kufanya pale anapovaa uzi wa Yanga.
Kuna maboresho makubwa Yanga inatarajiwa kufanya pale dirisha la usajili litakapofunguliwa, lengo likiwa kurejea makali kwenye michuano ya ligi ya mabingwa.