Kiungo mshambuliaji wa Yanga Allan Okello ameendelea kuzikusanya tuzo za nyota wa mchezo jana akichukua nyingine baada ya kuiadhibu vikali Namungo Fc.
Okello alifunga mabao mawili katika ushindi wa mbao 3-1 kwenye mchezo uliopigwa uwanja wa KMC Complex.
Hiyo ilikuwa tuzo ya nne katika mechi tano zilizopita ambapo nyota huyo wa Kimataifa wa Uganda amefunga katika kila mechi.
Okello amechukua tuzo katika mechi dhidi ya KMC, Coastal Union, Singida BS na leo Namungo Fc
Kama Yanga isingepoteza mchezo dhidi ya Dodoma Jiji pengine angetwaa tuzo hiyo pia kwani alipachika mabao mawili katika mchezo huo.
MVP wa ligi kuu 2025/26 tayari amepatikana...!

ADVERTISE HERE