Jumatatu May 25 2026 Yanga itashuka uwanja wa KMC Complex kuikabili Namungo Fc katika mwendelezo wa ligi kuu ya NBC.
Ni mchezo wa raundi ya 25 ambao Wananchi wanahitaji ushindi ili kurejea kwenye nafasi yao, kileleni mwa msimamo wa ligi.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi KMC Complex kuipa sapoti timu yao katika mchezo ambao ushindi ndio matokeo pekee ambayo Yanga inahitaji.
Wakati huu kauli ni moja tu, kila timu ishinde mechi zake..!

ADVERTISE HERE