Yanga, Nado lolote linaweza kutokea

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 May 2026
Yanga, Nado lolote linaweza kutokea

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga wanatajwa kumfuatilia kwa karibu kiungo mshambuliaji wa Azam FC Idd Suleiman 'Nado' ambaye amekuwa "moto" msimu huu.

Inelezwa Yanga inaongoza mbio za kumnasa mchezaji huyo ambaye mkataba wake na Azam FC unaelekea ukiongoni akiwa bado hajasaini mkataba mpya.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani ya mchakato wa usajili, Yanga tayari wameanza mawasiliano na wasimamizi wa mchezaji huyo ambaye pia yuko kwenye kikosi cha timu ya Taifa.

Nado (30) amekuwa katika kiwango bora msimu wa 2025/2026 akiwa miongoni mwa wachezaji muhimu ndani ya Azam FC.

Takwimu zake zinaonyesha mchango mkubwa akihusika kwenye mabao 11, akifunga mabao 8 na kutoa pasi 3 za mabao.

Uwezo wake wa kucheza pembeni, kupiga krosi maridhawa na kushambulia kwa kasi umeifanya Azam FC kunufaika naye katika michezo mingi ya ligi.

Kwa upande wa Yanga SC, Nado anaonekana kama chaguo muhimu katika mpango wao wa kuongeza nguvu kwenye winga, hasa kutokana na uzoefu wake ndani ya Ligi Kuu ya NBC na uthabiti wake katika msimu huu.

Akiwa mchezaji wa ndani, Nado anaweza kuiongezea Yanga upana wa kikosi kwani Wananchi watakuwa na nafasi nyingine ya kusajili winga mwingine wa kigeni.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
7h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
11h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
12h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
12h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’