Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanja wa KMC Complex kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida BS utakaopigwa saa 10 jioni.
Kamwe amesema kwa hatua ambayo ligi imefikia ni kila timu kushinda mechi zake ambapo Yanga kimahesabu itatetea ubingwa endapo watashinda mechi zote.
Amesema wachezaji wanahitaji sapoti kubwa ya mashabiki wao katika kila mchezo.
"KILA TIMU ISHINDE MECHI ZAKE, ndio kazi kubwa iliyo mbele yetu kwa sasa! kupambana kushinda kila mchezo wetu mbele."
"Hizi ni nyakati ambazo wachezaji wanatuhitaji sana mashabiki tusimame nao na tujae kwa wingi uwanjani kuwapa nguvu ya kutimiza malengo yetu"
"Mjulishe na Mwananchi Mwenzako .. Tusikose uwanja wa KMC mapema sana Saa 10:00 Jioni kupambania Pointi 3," aliandika Kamwe kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii.
Baada ya watani zao Simba kushinda mchezo dhidi ya Coastal Union, wamepanda kileleni mwa msimamo wa ligi lakini Yanga inaweza kurejea kwenye nafasi yake endapo haitapoteza mchezo dhidi ya Singida BS.