Mshambuliaji wa Pyramids Fc Fiston Mayele amejumuishwa kwenye kikosi cha DR Congo kitakachoshiriki michuano ya kombe la Dunia inayotarajiwa kuanza Juni 11 katika nchi za Canada, Mexico na Marekani.
Historia inakwenda kuandikwa kwa mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga kwenda kucheza kombe la Dunia.
Mayele ni mchezaji pekee katika kizazi cha sasa miongoni mwa waliocheza soka hapa Tanzania ambao wanakwenda kushuhudiwa pale Marekani wakiyapigania mataifa yao kwenye michuano mikubwa zaidi ya soka ngazi ya Mataifa.
Bila shaka DR Congo itapata uungwaji mkono mkubwa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na pasipo na shaka, Wananchi watakuwa bega kwa bega na mshambuliaji wao za zamani Mayele ambaye misimu michache nyuma aliyeweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa kombe la Shirikisho (CAFCC) akiwa na kikosi cha Yanga na kisha kuirudia rekodi hiyo kwenye michuano ya ligi ya mabingwa akiwa na Pyramids Fc.
