Baada ya kuhitimisha vyema robo fainali ya kombe la CRDB kwa ushindi dhidi ya JKT Tanzania na kutinga hatua ya nusu fainali, Yanga sasa inahamisha nguvu zake kuelekea ligi kuu ya NBC.
Kwa mujibu wa ratiba, Yanga inakabiliwa na mechi mbili kabla ya kupisha mapumziko ya kalenda ya FIFA.
Ijumaa May 22 Wananchi watakuwa dimba la KMC Complex kuikabili Singida BS katika mechi inayotarajiwa kuwa na upinzani mkali.
Jumatatu May 25 Yanga itarejea tena KMC Complex kumenyana na Namungo Fc katika mechi nyingine ngumu.
Katika mkakati wa kutetea taji la ligi kuu kwa msimu wa tano mfululizo, hakuna nafasi ya kufanya makosa, Yanga inahitaji kushinda mechi zote mbili.
Mchezo utakaofuata baada ya kalenda ya FIFA ni Juni 13 ugenini mkoani Kigoma dhidi ya Mashujaa Fc.