Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki na wanachama wa timu hiyo kuwaunga mkono wachezaji wao hata katika nyakati ngumu kuhakikisha wanakuwa na moyo wa kuipambania timu.
Kamwe ametoa kauli hiyo wakati akizungumzia kukosekana kwa nahodha wa Yanga Bakari Nondo Mwamnyeto kwenye mchezo wa robo fainali kombe la CRDB dhidi ya JKT Tanzania uliopigwa uwanja wa Isamuhyo jana.
"Mwamnyeto amekosekana leo sio kwa sababu ni mgonjwa hapana. Hakuwa katika hali nzuri kisaikolojia akamuombe mwalimu asimtumie"
"Ametumiwa meseji nyingi sana kwenye simu yake, nyingine sio nzuri. Timu inapokosa matokeo sio mashabiki tu mnaoumia hata wachezaji wanaumia sana."
"Nawaomba tuwaunge mkono wachezaji wetu katika nyakati zote, kwani nao ni binadamu zipo nyakati wanaweza wasifanye vizuri, tuwape moyo ili waendelee kupambana," alisema Kamwe