Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema mradi wa ujenzi wa uwanja wa Yanga utakamilika katika kipindi cha miezi 18 hadi 20.
Hersi amesema katika kipindi hicho anatarajia mradi utakamilika pamoja na kuzinduliwa na kuwa sehemu ya historia ya klabu.
"Matarajio yetu ni kwamba ujenzi wa uwanja huu utakuwa umekamilika na kuzinduliwa rasmi ndani ya kipindi cha miezi 18 hadi 20 ijayo."
"Tuna imani na matumaini makubwa kwamba mradi huu utakamilika kwa wakati uliopangwa na kuwa sehemu muhimu ya historia ya klabu yetu."
"Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa mara nyingine kwa Ghalib Said Mohamed pamoja na familia yake, kwa maamuzi yao makubwa na ya kizalendo waliyochukua kwa ajili ya kusaidia kutimiza ndoto ya muda mrefu ya Yanga," alisema Hersi
ADVERTISE HERE