Rais wa Yanga Injinia Hersi Said ametangaza mabingwa hao wa soka nchini kuingia makubaliano ya ubia wa umiliki wa uwanja kwa uwiano wa asilimia 50 kwa 50 na GSM Group.
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini makubaliano hayo iliyofanyika Makao Makuu ya Yanga, Jangwani jijini Dar es salaam, Hersi alisema Yanga itatoa ardhi kwa ajili ya mradi huo, huku mchango wa GSM Group ukiwa ni uwekezaji wa fedha kwa ajili ya ujenzi wa uwanja huo wa kisasa.
"Nathibitisha rasmi leo kuwa Young Africans S.C. imeingia katika makubaliano ya ubia wa umiliki wa uwanja wetu mpya kwa uwiano wa asilimia 50 kwa 50 na GSM Group."
"Tunamshukuru kwa dhati Ghalib Said Mohamed kwa moyo wake wa kizalendo na uamuzi wake wa kuweka usawa katika umiliki wa mradi huu mkubwa, licha ya kuwa yeye ndiye anayechangia sehemu kubwa zaidi ya uwekezaji wa kifedha."
"Kwa upande wa klabu, Young Africans S.C. itatoa ardhi kwa ajili ya mradi huo, huku mchango wa GSM Group ukiwa ni uwekezaji wa fedha kwa ajili ya ujenzi wa uwanja huo wa kisasa,β alisema Hersi