Baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Dodoma Jiji jana, kikosi cha Yanga kilirejea Dodoma usiku na tayari kimeondoka mkoani humo kurejea Dar es salaam.
Jumamosi, May 16 Yanga inakabiliwa na mchezo mwingine muhimu wa robo fainali kombe la CRDB dhidi ya JKT Tanzania.
Mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni jijini Dar es saalam.
Ni kwa mara ya pili Yanga inarudi Isamuhyo kucheza mwezi huu baada ya kucheza dhidi ya Simba May 03 mchezo wa ligi kuu uliomalizika kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2.
Baada ya kucheza mechi tatu dimba la Isamuhyo bila ya ushindi, wakati huu Wananchi wanahitaji ushindi ili kukata tiketi ya kutinga nusu fainali.
Matokeo tofauti na ushindi yatawashuhudia Wananchi wakitupwa nje ya michuano hiyo kwani ni mchezo ambao lazima mshindi apatikane.
Kama timu hizo zitatoka sare ndani ya dakika 90 basi changamoto ya mikwaju ya penati itatumika kupata mshindi.