Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewapa pole mashabiki na wanachama wa timu kufuatia kipigo cha mabao 3-2 dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa Airtel mkoani Singida.
Kamwe amewataka Wananchi kukubaliana na matokeo hayo kama sehemu ya mchezo na kusonga mbele kwani wamepoteza mchezo na sio malengo ya kutwaa ubingwa.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Kamwe ameandika ujumbe huu;
"Hii imeshaisha Wananchi. Kila mtu ana siku mbaya kazini. Prince Dube na Mwamnyeto tunaosikitika nao leo ndio waliotupa furaha sana kwenye Derby.
It’s Football. Malengo yetu hayakuwa kumaliza msimu bila kufungwa, Malengo ni UBINGWA. Tumeteleza leo lakini Alhamdulillah bado Ubingwa uko kwenye mikono yetu
Ni sisi kuamua, tuweke vichwa chini na kuendelea kuwachambua Players wetu Au tulibebe hili kwa kushukuru Tuendelee na uwanja wa mapambano
Tusicheze midundo ya wanafki wanaotuombea mabaya kila leo. Wao Yanga ikishinda, Ligi mbovu. Yanga ikifungwa, Usajili mbovu.
Niliposimama na kusema kuwa, Ligi ni ngumu na tunapaswa kuiheshimu Yanga inaposhinda nilimaanisha Football kwa kiwango kikubwa sana
Bado mechi 7 wanangu.. Tuna Faida ya pointi kileleni na sina mashaka kabisa, Tukisimama pamoja, Tutafanya vizuri In Shaa Allah
Daima Mbele Nyuma Mwiko"