Moalin afunguka maandalizi ya kuikabili Dodoma Jiji

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 May 2026
Moalin afunguka maandalizi ya kuikabili Dodoma Jiji

Kocha Mkuu wa Yanga Abdihamid Moalin amesema maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji yamekamilika.

Yanga itashuka uwanja wa Airtel mkoani Singida kesho Jumatano kuikabili Dodoma Jiji katika mchezo ambao wananchi wanazihitaji alama zote tatu ili kuendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi.

Moalin amesema wachezaji wote wako tayari isipokuwa beki Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' ambaye yuko chini ya uangalizi wa madaktari baada ya kurejea kikosini akitoka kwenye majeraha.

Moalin amesema anatarajia mchezo mgumu dhidi ya Dodoma Jiji lakini ana imani na ubora wa kikosi chake huku akiamini mazingira ya uwanja wa Airtel yatawapa faida kwa kuwa yanafanana na uwanja wa KMC Complex ambao wamekuwa wakicheza mechi zao za nyumbani.

Moalin amesema kila mechi iliyobaki ina umuhimu mkubwa hivyo watakwenda kucheza kwa tahadhari kubwa huku lengo likiwa kuibuka na ushindi.

“Maandalizi yamekuwa mazuri. Mzunguko kati ya mchezo uliopita na huu ni mfupi sana, hivyo tulipaswa kufanya kila linalowezekana kuhakikisha wachezaji wanapata muda wa kutosha wa kupumzika na kuwa tayari kwa mchezo wa kesho. Tunatarajia mchezo mgumu kama ule uliopita lakini naamini tuko tayari”.

“Utakuwa mchezo wenye ushindani mkubwa dhidi ya timu nzuri ya Dodoma Jiji. Nafikiri mazingira ya Uwanja yatatusaidia kidogo kwa sababu yanafanana na yale tuliyozoea kuchezea KMC. Pamoja na ratiba kuwa ngumu, tunajua tuna kazi ya kufanya hapa na tumekuja kwa ajili ya pointi tatu.”

“Wachezaji wote wako salama na tayari kwa mchezo isipokuwa tunamfuatilia Mohammed Hussein ambaye ameanza kurejea mazoezini baada ya kuumia. Tutategemea tathmini ya mwisho kutoka kwa madaktari kuona kama atakuwa tayari kucheza kesho."

"Pia ni jambo zuri kuwa Mudathir aliyekuwa kwenye adhabu ya kusimamishwa kurejea kikosini. Kila mchezo kuanzia sasa hadi mwisho wa msimu ni muhimu sana kwetu. Benchi la ufundi, wachezaji pamoja na uongozi wote tunafanya kazi kuhakikisha tunapata pointi tatu katika kila mchezo,” alisema Moalin

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
11h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
15h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
20h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
23h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’