Mwanahabari Ronnie Santos Mwine kutoka nchini Uganda ameripoti kuwa maafisa wa klabu ya Uturuki Fenerbahce wako nchini kwa siku nne wakimfuatilia nyota wa Yanga, Allan Okello.
Fenerbahce inayoshiriki ligi kuu ya Uturuki, imevutiwa kiungo huyo mshambuliaji wa Kimataifa wa Uganda ambaye alijiunga na Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo.
Okello amekuwa na kiwango cha kuvutia tangu alipojiunga na Wananchi akifunga mabao matano na kutoa pasi 7 za mabao mpaka sasa kwenye ligi.
Inaelezwa maafisa hao watakuwa jukwaani siku ya kesho wakati Yanga itakapokuwa ikichuana na Dodoma Jiji katika mchezo wa ligi kuu utakaopigwa uwanja wa Airtel Mtipa.
Endapo Fenerbahce watahitaji kumsajili Okello, watalazimika kukaa mezani na Yanga kwa ajili ya hatua zinazofuata. Mpaka sasa hakuna mazungumzo yoyote yaliyoanza baina ya pande mbili.
Okello alitua Yanga akitokea klabu ya Vipers Fc ya Uganda akisaini mkataba wa miaka miwili na nusu