Baada ya kuachana na kocha Pedro Goncalves, za ndaaani ni kuwa uongozi wa Yanga tayari umeanza kusuka mipango ya kumrejesha Kocha wa zamani wa timu hiyo, Nasreddine Nabi.
Nabi aliingoza Yanga misimu mitatu akifanikiwa kutwaa mataji mawili ya ligi kuu, CRDB na Ngao ya Jamii huku akiiwezesha Yanga kucheza fainali ya kombe la Shirikisho (CAFCC)
Kwa sasa hana timu baada ya kuachana na klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini aliyojiunga nayo mwanzoni mwa msimu huu akitokea AS FAR ya Morocco.
Licha ya kuondoka Yanga, Nabi ameendelea kuwa na mahusiano mazuri ya Wananchi na pengine ndio sababu mabosi wa Yanga wanafikiria kumrejesha.
Mpango wa kumrejesha kocha huyo raia wa Tunisia unatarajiwa kukamilishwa baada ya msimu huu kumalizika.
Makocha Abdihamid Moalin na Robert Mabedi ndio waliokabidhiwa mikoba ya kukamilisha mechi zilizosalia msimu huu ambapo jukumu lao kuu likiwa kuhakikisha Yanga inatetea mataji inayoshikilia yaani ligi kuu na kombe la CRDB.
Na hata kama Yanga itamrejesha Nabi, makocha hao huenda wakaendelea kusalia katika benchi la ufundi kama makocha wasaidizi.