Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza kumfuta kazi aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Pedro Goncalves raia wa Ureno.
Uamuzi wa kumfuta kazi Goncalves umetangazwa muda mfupi baada ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC uliopigwa uwanja wa KMC Complex Yanga ikipata ushindi mwembamba wa bao 1-0.
Kocha Msaidizi Abdulhamid Moarin amepewa jukumu la kuongoza benchi la ufundi akisaidiana na Patrick Mabedi hadi mwishoni mwa msimu.

ADVERTISE HERE