Kiungo mshambuliaji wa Yanga Allan Okello ameibuka kuwa mchezaji bora wa timu hiyo kwa mwezi April 2026.
Okello ameshinda tuzo hiyo (NIC player of the Month) baada ya kufanya vyema mwezi April akihusika katika upishi wa mabao pamoja na kufunga.
Hii ni tuzo yake ya kwanza tangu alipojiunga na Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo.

ADVERTISE HERE