Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limethibitisha waamuzi wa mchezo wa ligi kuu kati ya Simba dhidi ya Yanga utakaopigwa kesho Jumapili, May 03 katika uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo.
Mwamuzi wa kati atakuwa Hamza El Faruq, akisaidiwa na waamuzi wasaidizi Hamza En Nassri pamoja na Lahsen Agaou huku mwamuzi wa akiba akiwa Mustapha Kechaf wote wakitoka Morocco.
Mchezo huo wa watani wa jadi unatarajiwa kuchezwa Jumapili, Mei 3, katika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo Stadium uliopo Mbweni, Dar es Salaam, kuanzia saa 12 jioni.

ADVERTISE HERE