Beki kisiki wa Yanga Ibrahim Bacca amewataka mashabiki na wanachama wa timu hiyo kuendelea kuwa wamoja licha ya kupoteza mchezo wa fainali kombe la Muungano dhidi ya watani zao Simba hapo jana.
Bacca amewatia moyo Wanayanga akiwahakikishia kuwa watarejea katika furaha ya siku zote baada ya 'kutereza' hapo jana.
"Nyakati zote tunahitaji kua kitu kimoja, tunajua mnapitia mengi kwa hii hali ya jana ila tunapaswa kuheshi matokea"
"Ni vyema tuwe na subrah na kusahau mara moja kwani kesho yetu ni bora zaidi," aliandika Bacca kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii.
Katika mchezo huo Bacca aliondoka na tuzo ya mchezaji mwenye nidhamu.
Matokeo ya mchezo wa fainali kombe la Muungano dhidi ya Simba hayajawaumiza mashabiki tu, bali hata wachezaji wameonyesha kuumizwa na kipigo hicho kutoka kwa watani zao na kushuhudia wakipoteza taji la Muungano walilotwaa msimu uliopita.
Yanga ina takribani siku tatu za kujisahihisha kabla ya kukutana tena na Simba katika mchezo wa ligi kuu siku ya Jumapili, May 03 uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo.