Simba wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga katika mchezo wa fainali kombe la Muungano uliopigwa uwanja wa New Amaan Complex.
Mkwaju wa penati dakika ya 120 ndio uliozima ndoto ya Yanga kutwaa kombe la Muungano kwa msimu wa pili mfululizo.
Katika jitihada za kuondoa hatari langoni, winga Edmund John alimkwatua Clatous Chama katika eneo la hatari na hivyo mwamuzi kuamuru upigwe mkwaju wa penati ambao ulifungwa na Suleiman Mwalimu.
Ilikuwa mechi ngumu na yenye ushindani kwa dakika zote 120, zikiongezwa dakika 30 baada ya mchezo huo kumalizika kwa suluhu ya bila kufungana baada ya dakika 120.
Ulikuwa mchezo wa fainali ambao mshindi ilikuwa lazima apatikane na wakati huu ni Simba baada ya mfululizo wa matokeo mazuri kwa Yanga katika takribani mechi sita.