Nahodha wa Yanga Bakari Nondo Mwamnyeto ni sehemu ya kikosi kinachokamilisha maandalizi kuelekea mchezo wa fainali kombe la Muungano dhidi ya Simba utakaopigwa kesho Jumatano katika uwanja wa New Amaan Complex.
Mwamnyeto alikosa mechi mbili zilizopita akikabiliwa na changamoto za kifamilia. Hata hivyo 'kapteni' huyo wa makombe amerejea kwa wakati tayari kwa mechi nyingine ya fainali.
Inawezekana Mwamnyeto akawa nahodha aliyenyanyua makombe mengi zaidi katika historia ya manahodha wa Yanga.
Kwani tangu mwaka 2021, mikono ya Mwamnyeto imekuwa ikinyanyua mataji kila msimu.
Kuna msemo kutoka kwa mashabiki wa Yanga kuwa unapomuona Mwamnyeto uwanjani halafu ni fainali, jua kuna kombe linakwenda kabatini pale Jangwani.
Bila shaka msemo huo utatimia kwa mara nyingine siku ya Jumatano..!