EFM waiomba radhi Bodi ya Wadhamini Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Apr 2026
EFM waiomba radhi Bodi ya Wadhamini Yanga

Uongozi wa EFM na TVE wameomba radhi kwa Bodi ya Wadhamini ya klabu ya Yanga kutokana na maudhui yaliyoruka April 17 kwenye kipindi cha michezo cha Namba 10. Maudhui hayo yalitolewa na mchambuzi Wilson Oruma maarufu kam Mzee wa Jambia.

Akitoa taarifa kwa Wanahabari, Mkuu wa Idara ya Michezo EFM na TVE Abbisay Stephen Jr, amesema April 20 walipokea barua kutoka kwa Mwanasheria wa klabu ya Yanga iliyokuwa na taarifa ya kusudio la kuchukua hatua dhidi ya taasisi hiyo kutokana na kashfa, uchochezi dhidi ya klabu ya Yanga kupitia mchambuzi Wilson Oruma.

Abbisay amesema TVE haina utaratibu wa kurusha maudhui chonganishi yasiyo na mizania ya ushahidi.

"Kwa yote yaliyozungumzwa na mchambuzi Wilson Oruma kupitia majukwaa yetu ya mitandao ya kijamii, yale ni maoni yake binafsi na sio maoni ya kituo chetu"

"Ni kosa kutumia jukwaa letu kinyume na taratibu zinazofahamika. Mpaka sasa hatua mbalimbali zimechukuliwa ikiwemo kufuta maudhui yote yaliyochapishwa kwenye majukwaa mbalimbali pamoja na kumtaka mhusika kuomba radhi kupitia majukwaa hayo."

"Hata hivyo mhusika Wilson John Oruma hakuwa tayari kufanya hivyo kwa msimamo kwamba yuko tayari kwenda Mahakamani kwa utetezi wake zaidi," alisema Abbisay.

Yanga tayari imefungua shauri Mahakamani dhidi ya mchambuzi huyo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’