Baada ya Azam Fc kuichap KVZ mabao 2-0 katika mchezo wa pili wa robo fainali kombe la Muungano, sasa Dar es saalam derby itapigwa visiwani Zanzibar.
Ni mchezo wa nusu fainali ya michuano hiyo ambapo Yanga na Azam Fc zitaumana Jumamosi, April 25 uwanja wa New Amaan Complex.
Yanga ilikuwa ya kwanza kutinga nusu fainali wakiichapa Muembe Makumbi mabao 4-0 katika mchezo uliopigwa juzi.
Mkufunzi wa Yanga Pedro Goncalves ameweka wazi dhamira yake ni kuona wanatetea taji hilo kwa msimu wa pili mfululizo.
ADVERTISE HERE